Tembo GNU/Linux

Tembo ndio Mfumo wa tarakilishi wa kwanza wenye maonyesho ya tamaduni tofauti za Kiafrika na lugha ya asili ya Kiafrika katika hali msingi

Salama

Tunajali usalama wa data yako na ndio maana tunakuunganisha katika hali salama huku tukikupa uhuru wa kuongeza zana za kiusalama zinazoungwa mkono na mifumo mingine ya Linux

Nyepesi

Tunajali matumizi ya rasilimali yako na ndio maana tumeifanya Tembo GNU/Linux kuwa nyepesi sana na wenye uwezo wa kutumika kwenye mashine zenye upungufu wa rasilimali

Msaada

Pata msaada kutoka kwa jamii yetu kuhusu jinsi ya kuanza na maswala mengine kupitia jukwaa letu la Jamii na mifumo mingine ya mawasiliano kama vile SpotChat IRC na Telegram

Jinsi ya Kuchangia

Tembo GNU / Linux inasimamiwa na Swahilinux Microsystems na Jumuiya Wazi ya Swahilinux. Kuna njia kadhaa ambazo unaweza kushiriki kwenye mradi huu.
Uvumbuzi

Uvumbuzi

UANAPROGRAMU

Unaweza ukasaidia kujenga suluhisho la mahitaji ya ukuaji wa Afrika kupitia uanaprogramu

Ujanibishaji

Ujanibishaji

TAFSIRI

Unaweza kusaidia jumuiya ya Swahilinux kujanibisha programu hadi lugha ya Kiswahili au nyinginezo zenye uasili wa Kiafrika kwa kutumia msaidizi wa tafsiri "Kalimani" kwenye Telegram au Tafsiri kwenye wavuti

Ubuni

Ubuni

MANDHARI

Unaweza kuchangia kwa kubuni mandhari yanayosherekea utamaduni na ubunifu wa kiafrika

Wasiliana Nasi

Jihisi huru wa kuwasiliana nasi wasaa wowote na tutaweza kukujibu haraka iwezekanavyo

Tunapatikana Bara Afrika

Nairobi ,KE.

Barua Pepe

Maswala ya Umma

admin@swahilinux.org

Ubunifu na Uvumbuzi

obuya@swahilinux.org

Tuma Ujumbe